MKUU WA CHUO CHA TANGA TECHNICAL INSTITUTE (TTI) KINACHO MILIKIWA NA KKKT-DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI ANAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO MWEZI OKTOBA ( OCTOBER INTAKE), 2021. CHUO KIPO JIJINI TANGA, MKABALA NA SOKO LA TANGAMANO, NYUMA YA KANISA LA KKKT KANA (BARABARA YA NANE).

KOZI ZINATOLEWA KATIKA FANI ZIFUATAZO

ASTASHAHADA YA UONGOZI WA BIASHARA (BASIC CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION)

            Sifa za kujiunga:

 1. Alama nne za ufaulu katika kiwango cha D au zaidi Kidato cha Nne kwa masomo ambayo siyo ya dini. Kati hizo D nne mojawapo iwe ni ya Hisabati
 2. ASTASHAHADA YA UHASIBU NA FEDHA (BASIC CERTIFICATE IN ACCOUNTING AND FINANCE) 

Sifa za Kujiunga:

 1. Alama nne za ufaulu katika kiwango cha D au zaidi Kidato cha Nne kwa masomo ambayo siyo ya dini. Kati hizo D nne mojawapo iwe ni ya Hisabati, Commerce au Book-keeping

KOZI ZA STASHAHADA (DIPLOMA)

STASHAHADA YA UONGOZI WA BIASHARA (DIPLOMA IN BUSINESS  ADMINISTRATION) 

 Sifa za kujiunga:

 1. Astashahada ya Uongozi wa Biashara (Basic Certificate in Business Administration) ya ufaulu wa daraja la pili kutoka vyuo au taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
 2. Kidato cha Sita ufaulu wa angalau alama ‘E’ moja na Subsidiary moja au angalau ‘C’ tatu za Kidato cha Nne. Mwombaji lazima awe amefaulu somo la Hisabati au Biashara kwa ufaulu angalau alama ‘D’ katika Kidato cha Nne.
 3. Kama ‘E’ ya Kidato cha Sita sio somo la Hisabati au Biashara basi mwombaji awe angalau na alama ‘C’ katika Kidato cha Nne kwa somo hilo.

STASHAHADA YA UHASIBU NA FEDHA

(DIPLOMA IN ACCOUNTANCY AND FINANCE)

Sifa za kujiunga:

 1. Astashahada ya Uhasibu na Fedha (Basic Certificate in Accountancy and Finance) ya ufaulu wa daraja la pili kutoka vyuo au taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
 2. Kidato cha Sita ufaulu wa angalau alama ‘E’ moja na Subsidiary moja au angalau ‘C’ tatu za Kidato cha Nne. Mwombaji lazima awe amefaulu somo la Hisabati au Biashara kwa ufaulu angalau alama ‘D’ katika Kidato cha Nne.
 3. Kama ‘E’ ya Kidato cha Sita sio somo la Hisabati au Biashara basi mwombaji awe angalau na alama ‘C’ katika Kidato cha Nne kwa somo hilo.

Fomu za kujiunga zinapatikana Chuoni na kwenye tovuti ya Chuo www.tti.ac.tz

sharika za KKKT Kana, Makorora, Kisosora, Mikanjuni, Korogwe, Mombo, Lushoto,Kange, Handeni, Hale, Kowero Stationary Handeni na Manka Restaurant Barabara ya Saba Tanga.

Kwa mawasiliano zaidi piga:

 1. Mkuu wa Chuo -0718 911 334/0689488887
 2. Msajili – 0716 444 902/0783176000
 3. IT-0764105944/0685570696